MAANDALIZI

8:59 PM
Kabla ya harusi 

  1.  Kama utafanya engagement party basi panga siku kabisa
  2.  Utafanya kitchen party au bridal shower? Anza maandalizi 
  3.  Siku yako ya Send off 
  4. Unafikiria kufanya nini kwenye fungate? Fikiria maandalizi 


Harusi yako 

ZINGATIA 

Kwa kila malipo unayofanya usisahau kuandikishana au kuchukua stakabadhi (receipt) 
 
Ni vema kuwa na jalada ambapo utahifadhi habari zako zote kuhusiana 
na harusi yako 


-Fikiria unataka harusi ya aina gani, ndogo – watu wa karibu tu, kubwa na ya kifahari, ya kati kati, ukumbi wa nje? Ndani? 


-Kuna watu wanatoka mbali watakaohitaji malazi? Fanya mipango sasa 
o Ndugu jamaa na marafiki wanaweza kuwahifadhi? 
o Fanya booking na hoteli au Nyumba za wageni 

- Amua unataka kutumia kiasi gani cha pesa na wapi pa kukipata – Unaweza kupata msaada hapa 

- Chagua siku yako ya harusi, vigezo vyaweza kuwa muda wa watu wenu wa karibu au upatikanaji wa ukumbi au kanisa fulani, angalia kama ni siku ya sikukuu 

- Umeshaamua rangi ya harusi yako? 

- Umeshachagua wasimamizi wako? Wataarifu na kuwaeleza nini 
unategemea toka kwao 

- Je kuna mila au tamaduni zozote ambazo inabidi kuzitilia maanani? Fanya utafiti. Baadhi ya makabila hufanya hivi 

- Andaa ratiba ya harusi 

- Usiku wa harusi, fanya booking ya hotel 

- Paki kabisa vitu kwaajili ya usiku wa harusi, kama kuna 
vinavyokosekana fanya mipango ya kununua 

- Je utasafiri kwaajili ya fungato? Fanya booking sasa 
 Hakikisha una passport, viza, chanjo (kadi ya njano) 

SHEREHE 

Ukumbi – Maswali ya kuuliza kuhusu ukumbi 
- Anza kufikiria ukumbi, angalia hapa...omba ushauri kwa rafiki ndugu na jamaa 
- Chagua ukumbi wa harusi, baadhi iko hapa 
- Tembelea kumbi ulizozichagua kwa habari zaidi – set a date 
- Kama umeona ukumbi unaoupenda katika siku unayotaka, book huo ukumbi 
- Fanya malipo ya awali kama umeridhika na mahali hapo, kumbuka kuandikishana au kuchukua stakabadhi halali 

Maswali 
- Maegesho ya magari 
- Idadi ya juu ya watu wanaoweza kuwepo kwa wakati mmoja 
- Je wanatoa huduma ya chakula 
- Je wanatoa huduma ya vinywaji 
- Viti na meza je? 


Viti, meza na maturubai 
- Kama ukumbi hauji na viti na meza, fanya mipango ya kupata mahali 
pengine kama hapa 
- Kama ni ukumbi wa nje na hali ya hewa inafaa maturubai, inabidi 
kufanya mpango huo 

Chakula na huduma nyingine 
- Fikiria unataka kuserve chakula gani 
- Tafuta caters na kuwafanyia mahojiano, wengine wako hapa 
- Chagua cater kama umeridhika na mkubaliane bei na menu 
- Fanya malipo ya awali bila kusahau stakabadhi yako 

Vinywaji na wahudumu 
- Mpaka sasa unajua ni vinywaji gani unataka na kwa kiasi gani 
- Ukumbi unatoa huduma hii ya vinywaji? Je iko ndani ya budget yako? 
- Kama la tafuta mtu wa kukuletea vinywaji 
- Nani atahudumia, ukumbi unatoa wahudumu? Au mtu wa vinjwaji? 
- Fanya makubaliano, toa malipo ya awali 
- Usisahau Champagne, yenye kilevi au la? Angalia mapendekezo 

Keki 
- Keki, chagua aina unayotaka na nani atakayekutengenezea, anza na 
cater wako 
- Lipia keki yako 

MAVAZI NA UREMBO 

Gauni 
- Bi Harusi, anza kufikiria nguo yako ya harusi, unataka gauni la aina 
gani, agalia mifano hapa. Uliza maswali muafaka 
- Nguo ya bi harusi, umeshaamua ni aina gani? Au umeiona haswa 
unayoitaka? 
- Kama nguo yako ni ya kununua, nenda kaijaribu, kama ni ya kushona fikiria au pata ushauri juu ya mafundi wa nguo za harusi, unaweza 
kuanza na hawa 
- Gauni la harusi vipi? Kama umepima na umepata unachotaka lipia na chukua, kama ni la kushonesha anza kushona kwa fundi 
uliyemchagua, mtajie siku ya harusi ambayo ni mwezi mmoja kabla ya harusi 
- Kama gauni ni la kukodisha hakikisha umelipeleka kusafishwa dry cleaner 
- Anza kutafuta nguo za wasimamizi wako, watanunua au kushona? 

Shela and weaving au rasta 
- Mara nyingine gauni haliji na shela unayoitaka, anza kutafuta...angalia 
maduka ya nguo za harusi 
- Unafikiria kushonea weaving au kusuka rasta, aina gani na mtindo 
gani? Angalia mifano hapa 

Mapambo mengine 
- Hereni, Chain, bangili, viatu, gloves, pochi, vibanio 

SALUNI 
Nywele na vipodozi 
- Nywele, unataka ziwe vipi? Kama utasuka rasta panga siku kabisa na book msusi 
- Chagua saluni utakayopambiwa, ni vema kuchagua saluni inayotoa 
kuhuma zote unazohitaji 
- Fanya majaribio ya utakavyobana nywele 
- Unaweza kutaka kukata nywele pia, style gani? 

Ngozi na kucha 
- Fanya miadi ya kutengeneza kucha (pedicure, manicure) na 
kutengeneza ngozi (facial, waxing 
- Ni vema kufanya shughuli hizi mapema kabla ya siku ya harusi 

BWANA HARUSI 
Suti ya bwana harusi 
- Mkumbushe bwana harusi kufuatilia nguo yake na m(wa)simamizi wake 

Mapambo ya bwana harusi 
- Cuflinks, viatu 

KANISANI/MSIKITINI/KAMISHNA 
- Andikisha harusi yenu walau mwezi mmoja kabla ya siku 
- Kuna semina mbalimbali makanisani na misikitini kwa maharusi 
watarajiwa, chunguza ni lini na fanya mpango kuhudhuria 

MAUA NA MAPAMBO 
- Wapambaji – angalia baadhi ya mapambo 
- Chagua uliyeridhishwa naye na kukubaliana aina ya mapambo na 
maua 
- Usisahau maua ya bibi harusi kama utapenda 
- Ingia naye makubaliano na lipia gharama za awali 


MC na MUZIKI 
- Muziki na msema chochote, angalia hawa, kutana nao kuwaeleza 
unataka sherehe ya aina gani. 
- Wimbo wa kufungulia dansi – your wedding song hakikisha MC au bendi ya muziki wanao 
- Kama umeshachagua MC, na muziki, book na fanya malipo ya awali, ni vyema kuandikishana 

PICHA ZA MNATO NA VIDEO 
- Angalia baadhi yao na kazi zao hapa 
- Kuna wale ambao wataweka picha zako kwenye album yako ndani ya hii tovuti yako na kuwa rahisi kushirikisha ndugu, jamaa na marafiki. 
- Umeridhishwa na mmoja? Panga kuonana naye na kufanya 
makubaliano 

KADI NA MIALIKO 
Invitation cards 
- Anza kufikiria orodha ya wageni wako wageni wako 
- Orodhesha wageni wako, chukua majina toka kwa wazazi wa pande zote mbili na yenu pia 
- Kamilisha orodha yako ya wageni, umetumia msaidizi? 
- Kuna maneno maalumu unataka kuandika kwenye kadi? Anza 
kuyaandaa 
- Nunua au tengeneza kadi za mwaliko, hawa wanaweza kukusaidia 
- Tuma ujumbe kwa watu walioko katika orodha yako kuhusu siku yako ya harusi, ili wasifanye mipango mingine katika siku hiyo (Save this date) 
- Tuma kadi za mwaliko walau mwezi mmoja kabla ya harusi 
- Andaa ratiba ya harusi na kuiprint, inaweza kuambatana na kadi za mwaliko 

Thank you notes/chocolates/ handkerchiefs 

PETE 
- Anza kutafuta pete unazotaka 
- Amua ni pete zipi, zinapatikana duka gani? fanya vipimo 
- Nunua pete 

USAFIRI 
- Tengeneza ratiba ya usafiri na ni magari mangapi na ya aina gani 
yanatakiwa 
- Tafuta usafiri, kama ni wa kukodi ni vyema kuyaona magari. Wanaotoa huduma hii 
- Fanya malipo ya awali na kukubaliana mpango wa safari 

ZAWADI 
- Unataka zawadi gani, chagua zawadi zako ili usipate seti kumi za 

sahani na vikombe, ziorodheshe hapa 

MENGINEYO 
- Kama kuna maonesho yoyote maalumu yaandae na kuyaweka katika ratiba 
- Usisahau kitabu cha wegeni kama utataka 
- Jiandae mapema kwa fungate, nunua vitu utakavyohitaji mapema 
kabla ya harusi, vipaki kabisa Kwa kila malipo unayofanya usisahau kuandikishana au kuchukua stakabadhi (receipt) 
Mara mahali, saa na utaratibu utakapokua kamili, wasiliana na watoa huduma wako wote ili wajue jinsi ya kutekeleza kazi zao na 
kufanikisha shughuli yako 

Gawa majukumu: 
Kukaribisha wageni 
Kupokea zawadi 
Kutambulisha ndugu 
Kumalizia malipo kwa watoa huduma wako – mtu huyu awe unayemuamini, si ajabu mtakua naye katika safari yote ya kuandaa shughuli yako 

Wedding theme/Dhana za harusi 
Unajua kwamba unaweza kuipa harusi yako dhana Fulani? Hebu angalia mifano: 
Classic white wedding 
Traditional wedding 
Beach wedding 
Cocktail wedding 

Barbecue

Src:Harusi Yangu

Toa maoni yako hapo chini, na kama una swali lolote karibu


8 comments:

  1. Yote uliyosema NI muhimu Sana. Vijana wengi hukwepa mlolongo wa Mambo hayo eti wanaepuka gharama na kuchukuana haraka haraka. Nashauri Kila mtu ajipange awezavyo.

    ReplyDelete
  2. Imekaa vizuri ndugu.Tuombe uzima kuna baadhi ya huduma tutaziitaji tutakutafuta.

    ReplyDelete
  3. Najivunia kusoma habari hii naamini itanisaidia

    ReplyDelete
  4. mnatoa huduma ya ku-plan tukio zima la sherehe ya harusi. na kama mnafanya naomba maelekezo ya huduma zenu kwa ujumla.

    ReplyDelete

Need an Invite?

Want us to participate in your wedding event? Leave us a message.

Name Email * Message *

Our Location